iqna

IQNA

IQNA – Mkurugenzi mtendaji wa toleo la kwanza la mashindano ya Qur'ani ya kitaifa ya ‘Zayin al-Aswat’ (mapambo ya sauti) amesema kuwa katika mashindano mengi ya Qur'an, kila kitu huisha kwa sherehe ya kufunga na kuwatuza washindi na sasa sekretarieti ya tukio hili la Qur'an inalenga kuandamana na washiriki kupitia mawasiliano endelevu na yenye tija ili kuwafikisha katika viwango vya kitaalamu na vya kimataifa.
Habari ID: 3481314    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/01

IQNA – Ahmad Abolqassemi, Qari mashuhuri kutoka Iran, amesisitiza uwezo wa kipekee wa nchi hiyo katika uwanja wa usomaji wa Qur’ani Tukufu, akipendekeza kuandaliwa mashindano mapya ya kipekee ya “fainali ya mabingwa” kwa washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, yatakayofanyika nchini Iran.
Habari ID: 3481300    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29

IQNA – Libya imetangaza washindi wa Tuzo ya 13 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu, iliyofikia tamati mjini Benghazi kwa ushiriki wa zaidi ya mataifa 70.
Habari ID: 3481299    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29

IQNA – Toleo la kwanza la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya Iran ya “Zayin al-Aswat” (mapambo ya sauti) linatarajiwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Qom, likijumuisha makundi matatu kuu, waandaaji walitangaza.
Habari ID: 3481298    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/28

IQNA-Mashindano ya sita ya kuhifadhi, kusoma, na Tajwidi ya Qur’ani Tukufu nchini Morocco yameingia katika hatua ya mwisho, yakifanyika kuanzia Ijumaa katika mji wa Fez.
Habari ID: 3481290    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/27

IQNA – Majina ya wale wanaostahiki kushiriki katika hatua ya fainali ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran yametangazwa.
Habari ID: 3481277    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/24

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya Mfalme Salman bin Abdulaziz ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume (SAW) barani Afrika imehitimishwa kwa hafla rasmi iliyofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Habari ID: 3481271    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/23

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 39 ya Kitaifa ya Qur’ani na Etrat kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Iran imepangwa kufanyika katika mji wa kati wa Isfahan.
Habari ID: 3481268    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/22

IQNA – Mji wa Benghazi ulioko kaskazini mashariki mwa Libya ni mwenyeji wa toleo la 13 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya nchi hiyo.
Habari ID: 3481261    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21

IQNA – Taasisi ya Mohammed VI ya Maulamaa wa Afrika inatarajiwa kuandaa fainali za mashindano yake ya sita ya kuhifadhi, kusoma, na tajwidi ya Qur’ani Tukufu kuanzia tarehe 26 hadi 28 Septemba.
Habari ID: 3481260    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21

IQNA – Hatua ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu imeanza Alhamisi katika mji mkuu wa Afrika Kusini, ikiwakutanisha washiriki kutoka nchi 29.
Habari ID: 3481250    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/19

IQNA – Sheikh Abdel Fattah Taruti, qari mashuhuri wa Misri na mjumbe wa majopo ya majaji wa mashindano ya Qur’ani ya “Dawlat al-Tilawa”, amesema kwamba kila mshiriki katika mashindano hayo ni mshindi, hata ikiwa hatofika katika hatua ya mwisho.
Habari ID: 3481241    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/16

IQNA – Mashindano ya Qur’ani yalifanyika kwa ajili ya wanafunzi mahiri waliokuwa wakihudhuria kozi za Qur’ani za majira ya kiangazi zilizoandaliwa na Jumuiya ya Kisayansi ya Qur’ani Tukufu chini ya usimamizi wa Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Abul-Fadhlil Abbas (AS).
Habari ID: 3481166    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/01

QNA – Toleo la 19 la Tuzo ya Kimataifa ya Mohammed VI ya Kuhifadhi, Kusoma, Tajweed, na Tafsiri ya Qur'ani lilifunguliwa Jumanne, Agosti 26, mjini Rabat, Morocco.
Habari ID: 3481150    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/28

IQNA – Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamu yanajitahidi kuimarisha uhusiano kati ya washiriki duniani kote badala ya kuwa mashindano ya muda mfupi pekee, amebaini mtaalamu.
Habari ID: 3481148    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/28

IQNA – Hatua ya kuchagua wawakilishi wa Iran katika Mashindano ya Saba ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu imefanyika katika Shirika la Qur’ani la Wanazuoni wa Iran, Jumanne.
Habari ID: 3481141    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26

IQNA – Mashindano ya kitaifa ya kuwania nafasi ya kushiriki katika Juma la 27 la Qur’ani Tukufu nchini Algeria yameanza leo Jumanne, kulingana na Wizara ya Mambo ya Kidini na Wakfu.
Habari ID: 3481140    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26

IQNA – Saudi Arabia imetangaza washindi katika makundi matano ya Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Mfalme Abdulaziz yaliyofanyika mjini Makkah.
Habari ID: 3481116    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/21

IQNA – Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu ya Mfalme Abdulaziz yanatarajiwa kufikia tamati kwa hafla maalum itakayofanyika mjini Makkah siku ya Jumatano.
Habari ID: 3481110    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/20

IQNA – Washiriki wa Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdulaziz wametembelea misikiti ya kihistoria na maeneo ya turathi katika mji wa Madina, kama sehemu ya programu ya kitamaduni iliyoandaliwa na mamlaka za Saudi Arabia.
Habari ID: 3481108    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/19